Genesis 35:22-26

22Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili.

Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:

23Wana wa Lea walikuwa:
Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo,
Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni.
24 aWana wa Raheli walikuwa:
Yosefu na Benyamini.
25 bWana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa:
Dani na Naftali.
26 cWana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa:
Gadi na Asheri.
Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.

Copyright information for SwhNEN